Nenda kwa yaliyomo

Simba S.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simba S.C.
Jina la utaniMnyama
Imeanzishwa1936
UwanjaBenjamin Mkapa Stadium
(Uwezo: 62,000)
MwenyekitiMurtaza Mangungu
MenejaPatrick Rweyemamu
KochaDimitar Pantev
LigiNBC Premier League
Tovutitovuti ya klabu

Simba Sports Club ni timu ya soka iliyo na makao makuu katika mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo ilianzishwa mwaka 1936, ikiitwa kwanza Eagles na baadaye tena iliitwa Dar Sunderland. Mwaka 1971 ikaibadilisha jina lake kabisa na kuitwa, Simba Sport Club (ambalo linamaanisha Lion kwa Kiingereza).

Simba Sports Club ni mojawapo ya timu kubwa ya mpira wa miguu nchini Tanzania, wapinzani wao wanaitwa Younɡ Africans.

Ni mabingwa wa taifa mara 18 tena ni mabingwa mara 6 katika kombe la Kagame.[1]

Mechi zao za nyumbani zinachezwa kwenye viwanja viwili, Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa.

Kufikia Oktoba 2025, timu inanolewa na kocha kutoka Bulgaria Dimitar Pantev[2].

Mabadiliko ya utawala

Klabu ya soka ya Simba imesajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 12 ya baraza la michezo la taifa ya mwaka 1967 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 1971. Katiba ya sasa ya timu ya Simba iliandikwa mwaka 2018 na kupitishwa tarehe 20 mayi 2018 na msajili wa vyama vya soka na klabu, na kisha kusajililiwa na wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA). Safari ya timu ya soka ya Simba kuelekea mabadiliko ilianza mwaka 2016 ambapo Kamati kuu kwa wakati ule ilibaini kwamba klabu iliendeshwa nje ya misingi na dira yake, hivyo kupelekea kushindwa kutimiza matarajio ya wadau wake, jambo lililopelekea kuwepo na ulazima wa kufanya mabadiliko ya kisasa kwa ajili ya maendeleo ya klabu.

Kamati kuu iliteua wajumbe wa kujitolea na wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha kutetereka kwa klabu ikiwemo kuzorota kwa uongozi, maendeleo hasi ya kiufundi, hali mbaya ya kifedha na kisha kupendekeza namna ya kufanya mabadiliko ili kuinusuru klabu. Kutokana na ripoti kamili na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya mabadiliko mnamo Septemba 2016; Klabu ya soka ya Simba ipo katika mchakato wa mabadiliko hayo kwa kubadili mfumo wake wa kisheria na kiuendeshaji kutoka mfumo wa wanachama na kuwa kampuni ya dhima ya umma inayojulikana kama Simba Sports Club Limited, ambayo imeundwa na pande mbili; wanachama wakimiliki asilimia 51 ya hisa ambapo kati ya hizo, asilimia 10 zimelipiwa zote na kubaki asilimia 41, huku mwekezaji akimiliki asilimia 49. Mabadiliko yote yalifanyika kupitia mchakato wa wazi wa kutangaza zabuni na kusimamiwa na kamati maalumu ya uwekezaji wa klabu.

Kabla ya kupokea zabuni, kamati maalumu ya uwekezaji ya timu ya soka ya Simba, iliteua kamati ya kufanya tathmini ambayo ilijumuisha wajumbe watano wakiwa na jukumu la kufanya tathmini na kuleta mapendekezo kwenye kamati ya uwekezaji kwa kubainisha zabuni gani ilikuwa na faida kiuchumi. Zabuni iliyopata tathmini ya juu zaidi ilikuwa ni ya ndugu Mohammed Dewji ambayo ilikubalika kwa kukidhi vigezo vya tathimini kama vilivyobainishwa kwenye nyaraka za zabuni.

Mchakato wa kufanya tathmini ulipitia hatua zifuatazo: Tathmini ya hisa, mkakati wa kiufundi, mpango wa kifedha na mwisho ilikuwa hatua ya makubaliano. Tarehe 2 Novemba 2018, Simba Sports Company Limited ilijumuishwa na kuwa na wanahisa wawili wakijulikana kama Simba Sports Club Holding company limited ikimiliki asimilia 10 ya hisa zilizolipiwa na asilimia 41 ambazo hazijalipiwa jumla hisa 51, na Mo Simba Company Limited ikimiliki asilimia 49 ya hisa zikiwa zote zimelipiwa. Mchakato wa mabadiliko haya upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Kama sheria inavyoelekeza katika kifungu cha 11 cha sheria ya ushindani wa biashara ya mwaka 2003; klabu ya soka ya simba: Imeomba idhini kutoka tume ya ushindani wa biashara kuhakikisha kwamba mchakato wa mabadiliko hauangukii katika ujumuishaji wa hisa (merger and acquisition) Inazingatia kanuni za mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) kuhusu uhamishaji wa mali Imeanza zoezi la uhakiki ili kutambua wanachama hai wa klabu ambao watanufaika na hisa. Mchakato huu unaendelea vizuri na wanachama pamoja na mashabiki wa timu ya Simba wameanza kushuhudia mabadiliko chanya ndani ya klabu yao pendwa. labu

Utawala

Simba Sports Club imebadilisha utawala au usimamizi wake kutoka kutawaliwa na mashabiki na badala yake kusimamiwa na mwanahisa aitwae Mohammed Gulam Dewji.

Katika muundo huu wa utawala wa Simba Sports Club imeuza hisa zake 49% kwa Mohammed Gulam Dewji huku wanachama wa Simba wakibakiwa na 51%.

Misimu

2024/25

Baada ya kutokufanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo, Simba iliamua kufanya mabadiliko ya lazima ili kurudisha ushindani wake ulikua nao kwa misimu ya nyumba. Moja ya mabadiliko ni kurudi kwa Mohamed Dewji kuwa mwenyekiti wa wa Bodi ya wakurugeni, akichukua nafasi kutoka kwa Saidi Abdallah Tryagain.[3] Baada ya kurudi, Simba ilishuhudia mabadiliko katika kikosi chake ikiwa ni pamoja na kubadili Benchi la ufundi, ambapo Fadlu Davis alitajwa kuwa Kocha mkuu[4] na kusajili wachezaji wengine wapya, Ambao walitangazwa kupitia kurasa rasmi za timu na baadae kuonekana kwenye siku ya Simba Day Agosti 3 2024.[5]

Simba walianza msimu mpya wa 2024/25 kwa kuweka kambi nchini Misri[6]. Ambapo walicheza michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya maandalizi. Japo Simba walianza msimu kwa kupoteza dhidi ya wapinzani wao wa Jadi Yanga kwenye mechi ya nusu fainali Ngao ya jamii[7], Mashabiki na uongozi kwa ujumla wameonyesha kuridhishwa na mabadiliko ya timu kwa ujumla, huku wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mechi za kimataifa na za nyumbani.

Mashindano ya Ndani
  • Ligi Kuu ya NBC

Katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara maarufu kama NBC Premier league, Simba walimaliza nafasi ya Pili nyuma ya wapinzani wao wa jadi kwa tofauti ya alama Nne[8]. Mchezo wa mwisho wa Msimu baina ya timu hizi mbili ndio ulioamua mshini wa ligi kwa msimu huo ambapo Yanga alishinda magoli 2-0[9], mchezo huo uliahirishwa mara mbili kutokana na sababu mbali mbali, hali iliyopelekea kuwa chezo wa mwisho na wa kufunga ligi[10].

  • Mashindano ya FA

Katika mashindano ya FA yanayotambullika kama CRD Federation cup, Simba iliishia hatua ya nusu fainali. Katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja wa Tanzanite kwa raha, Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1[11] dhidi ya Singida Big Stars ambao walicheza fainali na timu ya Yanga[12].

Wachezaji

Kikosi Cha sasa Kuanzia Julai 2025[13]

No Nchi Nafasi Jina la Mchezaji
26 Gine GK Moussa Camara
22 Tanzania GK Yakoub Suleiman Ali
12 Tanzania DF Shomari Kapombe
23 Afrika Kusini DF Rushine De Reuck
14 Tanzania DF Abdulrazack Hamza
2 Kamerun DF Chamou Karaboue
4 Tanzania DF Vedastus Masinde
31 Tanzania DF Wilson Nangu
5 Tanzania DF Anthony Mligo
12 Tanzania DF Shomari Kapombe
15 Tanzania DF David Kameta
21 Tanzania MF Yusuph Kagoma
8 Senegal MF Alassane Kante
30 Gine MF Naby Camara
19 Tanzania MF Mzamiru Yassin
37 Tanzania MF Hussein Semfuko
35 Afrika Kusini MF Neo Maema
18 Tanzania MF Morice Abraham
10 Côte d'Ivoire MF Jean Charles Ahoua
33 Tanzania MF Awesu Ally Awesu
7 Zambia MF Joshua Mutale
34 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MF Ellie Mpanzu
17 Kenya MF Mohammed Bajeber
36 Tanzania MF Ladaki Chasambi
11 Uganda FW Steven Mukwala
38 Tanzania FW Denis Kibu
40 Tanzania FW Selemani Mwalimu
3 Ghana FW Jonathan Sowah

Matokeo kwenye Mashindano ya CAF

Ligi ya Mabingwa Afrika: Ushiriki mara 12

  • 2002 – Hatua ya Awali
  • 2003 – Hatua ya Makundi
  • 2004 – Hatua ya mtoano
  • 2005 – Hatua ya Awali
  • 2008 – Hatua ya Awali

Kombe la Vilabu Bingwa Vya Afrika: Ushiriki mara 9

  • 1974 – Nusu Finali
  • 1976 – Hatua ya pili
  • 1977 – Hatua ya pili
  • 1978 – Hatua ya pili
  • 1979 – Hatua ya Pili
  • 1980 – Hatua ya Pili
  • 1981 – First Round
  • 1994 – Quarter-Finals
  • 1995 – Hatua ya Pili

Kombe la Shirikisho Afrika: Ushiriki mara 6

Kombe la CAF: Ushiriki mara 2

Marejeo

  1. Tanzania - RSSSF
  2. Joel Thomas (2025-10-03). "Unamfahamu, Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC? Hizi hapa rekodi zake, mifumo na mafanikio" (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-10-04.
  3. https://www.mwananchi.co.tz/mw/michezo/mo-dewji-abadili-gia-angani-arudi-simba-sc-3002626
  4. https://ippmedia.com/the-guardian/sports/football/read/fadlu-davids-poised-to-be-named-as-simbas-head-coach-2024-07-04-174634
  5. https://newtimestanzania.com/simba-day-ni-agosti-3-2024/
  6. https://www.mwanaspoti.co.tz/ms/soka/simba-yajichimbia-kambi-ya-kishua-yaanza-na-pumzi-stamina-4686256
  7. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/sports/yanga-beat-simba-to-secure-spot-in-community-shield-final-against-azam-fc-4719350#:~:text=Young%20Africans%20(Yanga)%20have%20once,at%20the%20Benjamin%20Mkapa%20Stadium.
  8. https://ligikuu.co.tz/nbc-premier-league/season-2024-2025/
  9. https://www.bbc.com/swahili/articles/cy0w5j55l80o
  10. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/sports/derby-drama-yanga-simba-rescheduled-again-now-slated-for-june-25-5080710#:~:text=The%20match%2C%20which%20has%20already,2025%2C%20at%20the%20same%20venue.
  11. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/sports/simba-sc-crashed-out-of-federation-cup-by-singida-black-stars-in-3-1-thriller-5064132
  12. https://www.jamiiforums.com/threads/full-time-young-africans-sc-2-0-singida-black-stars-crdb-federation-cup-final-new-amaan-stadium-29-06-2025-yanga-bingwa.2357729/
  13. "Tanzania - Simba Sports Club - Results, fixtures, squad, statistics, photos, videos and news - Soccerway". int.soccerway.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 2021-01-07.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje