Maafikiano ya Utambuzi
Maafikiano ya utambuzi hufanyika wakati nchi mbili au zaidi au taasisi nyingine zinatambua maamuzi au sera za nchi nyingine, kwa mfano katika taaluma. Maafikiano ya utambuzi wa kila upande ( MRA ) ni makubaliano ya kimataifa ambayo nchi mbili au zaidi zinakubali kutambua tathmini, maamuzi au matokeo (kwa mfano vyeti au matokeo ya mtihani).
Makubaliano kama haya hutumiwa sana sana kwenye bidhaa, kwa mfano katika udhibiti wa ubora . Hata hivyo, pia yanatumika kwa mikataba ya utambuzi wa hitimisho za kitaaluma na maamuzi yanayohusiana na masuala ya uhalifu.
Maafikiano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
[hariri | hariri chanzo]Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki imetoa nafasi ya kuwepo kwa makubaliano ya kila nchi katika jumuiya kutambua na kutambuliwa hitimisho za kitaaluma na sifa za kitaaluma. Makubaliano yaliyofanywa ni katika taaluma za uhasibu, uhandisi, usanifu majengo na sayansi ya tiba ya wanyama. Wananchi wa nchi zilizosaini makubaliano hayo wana haki ya kufanya kazi katika nchi nyingine iliyosaini bila kuwekewa vikwazo[1].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mutual Recognition Agreements". www.eac.int. Iliwekwa mnamo 2025-08-21.