Nenda kwa yaliyomo

Dave Sim

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dave Sim (amezaliwa 17 Mei 1956) ni mchoraji na mchapishaji wa katuni kutoka Kanada, anayejulikana kwa kitabu chake cha katuni kinachoitwa "Cerebus." Pia, amekuwa akijulikana kwa ubunifu wake wa kisanaa, kutetea haki za waandishi wa katuni, na mitazamo yake ya kisiasa na kifalsafa ambayo mara nyingi imezua mijadala.

Sim alipata umaarufu kupitia Cerebus, iliyozinduliwa mwezi Desemba 1977. Hapo awali, Sim aliibuni kama kukejeli kitabu cha katuni Conan the Barbarian na vitabu vingine vya katuni za upanga na uchawi, lakini baada ya miaka miwili alianza kuichukulia mfululizo huo kama kazi inayojitegemea ambayo ingekuwa na matoleo 300 na kugawanywa katika riwaya. Kufikia Machi 2004, kazi hiyo yenye kurasa 6000 ilipokamilika, pia alikuwa amejiingiza katika masuala ya siasa, na uchambuzi wa harakati za jinsia, huku akizidi kuwa wa kifasihi na majaribio katika simulizi na sanaa yake. Baada ya hapo, Sim alifanya kazi kwenye kumbukumbu za Cerebus, na akazalisha vitabu vya katuni inayoitwa Glamourpuss, ambacho vinaelezea historia ya katuni za picha halisi, na Judenhass, kuhusu mauaji ya kimbari ya Kiyahudi (Holocaust).

Mnamo, mwaka 1977, Sim alishirikiana na mchumba wake wa baadaye, Deni Loubert, kuanzisha kampuni ndogo ya uchapishaji inayoitwa Aardvark-Vanaheim. Baada ya wanandoa hao kuachana katikati ya miaka ya 1980, machapisho mengi ya kampuni hiyo yalihamishiwa Renegade Press ya Loubert. Baadaye, kampuni ya uchapishaji ilimilikiwa pia na mshirika wa ubunifu wa Sim, Gerhard, ambaye alisitisha ushirikiano wao na kuuza hisa zake kwa Sim mwaka 2007.

Mnamo, mwaka 1988, Sim alisaidia kuunda Creator's Bill of Rights. Pia, ameikosoa matumizi ya hakimiliki katika kuwabana wabunifu, na amepanga kazi zake zote ziwe mali ya umma baada ya kifo chake. Tayari Sim ameweka moja ya kazi zake, Judenhass, katika umiliki wa umma.[1]

  1. "Weekly Update #56: Judenhass In The Public Domain," A Moment of Cerebus (7 November 2014).
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dave Sim kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.